Klabu ya Simba imetishia kugomea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Timu hiyo imedai itagomea mchezo huo kama mabango ya GSM yatawekwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mapema leo Simba ilimzuia kocha wake Pablo Franco kuzungumza kwenye Mkutano na Wanahabari wakipinga uwepo wa mabango ya GSM kwenye ukumbi, wakishinikiza yatolewe kabla wao kuzungumza, TFF iligoma kutoa mabango hayo
Mpaka wakati huu tayarii mabango ya GSM yamepamba uwanja wa Benjamin Mkapa. GSM ni moja ya wadhamini wa ligi kuu hivyo huwezi kuzuia mabango yao katika tukio lolote linalohusiana na ligi
Hata hivyo wadadisi wa mambo wanasema Simba inajaribu kutengeneza mazingira ya kuwaaminisha Yanga kuwa mchezo huo hautakuwepo ili kuwavuruga pale watakapoibuka uwanja wa Benjamin Mkapa pasipo kutarajiwa
Mabosi wa Yanga wameshashitukia 'mind-game' hizo wanazocheza Simba, wanaendelea na maandalizi tayari kwa mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 11 jioni