Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa, utakuwa na ushindani mkali
Nabi amesema pamoja na Yanga kupewa nafasi ya kushinda, yeye kama kocha anaamini mchezo huo una uwiano wa 50/50 na kuwa timu itakayocheza vizuri ndio itashinda
"Mchezo wa Derby ni mgumu na hautabiriki, kuna watu wanaipa nafasi kubwa Yanga ya kushinda lakini mpira hauko hivyo, mechi ya Derby ni 50/50. Inachokakiwa kuwaheshimu wapinzani na kutimiza majukumu vizuri uwanjani. Wachezaji wetu wapo vizuri kimwili na kiakili lengo letu ni kuhakikisha tunashinda," alisema Nabi
Wakati Nabi akifika kuzungumza na wanahabari, Maafisa wa Simba wao walifika katika ukumbi wa mikutano lakini katika hali ya kushangaza waligoma kuzungumza
Imeelezwa maafisa hao waligomea uwepo wa bango la GSM ambaye ni Mdhamini mwenza wa ligi kuu ya NBC