Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kikosi kinaendelea vyema na maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, Disemba 11 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Bumbuli amesema katika maandalizi yao wanamkosa mchezaji mmoja tu, Yacouba Songne ambaye anauguza majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti
"Tunaendelea vyema na maandalizi, wachezaji wote wako sawa, tunamkosa mchezaji mmoja tu, Yacouba Songne ambaye kila mmoja anafahamu alifanyiwa upasuaji wa goti"
"Jumamosi tulicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Friends Rangers (Yanga ilishinda 1-0) kuwapa mazoezi wachezaji ambao hatukuwatumia mkoani Mbeya, Jumapili tukawa na siku maalum ya burudani, tumerejea mazoezini jana Jumatatu"
"Mwezi huu wa Disemba tutacheza mechi tano hivyo tunafanya maandalizi kwa ajili ya mechi zote ukiwemo mchezo dhidi ya Simba Jumamosi," alisema Bumbuli