Jana ilikuwa siku ya mapumziko kwa wanafamilia wa Yanga ambapo wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na wafanyakazi wa Yanga walikutana pale White Sands Hotel kufurahi na kubadilishana mawazo

Leo timu inaendelea na maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, Disemba 11 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga ambao unapigwa katika kipindi kizuri sana, Yanga ikiwa katika ubora
Katika misimu mitatu, minne nyuma Yanga ilikuwa ikiingia kwenye mchezo dhidi ya Simba ikiwa katika presha kubwa
Lakini wakati huu mambo yamebadilika, ni Simba ambao wataingia kukabiliana na Yanga wakiwa kwenye presha kubwa
Aidha ile hofu ya mchezo huo kusogezwa mbele haipo tena baada ya jana kocha mkuu wa timu ya Taifa Kim Poulsen kuwaacha wachezaji wa Yanga na Simba kwenye kikosi chake ambacho kitacheza na Uganda mchezo wa kirafiki kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru