Kikosi cha Yanga kimerejea kambini jana kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi ijayo, Disemba 11 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Baada ya kurejea kutoka mkoani Mbeya ambao waliweza kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza, wachezaji walipewa mapumziko ya siku mbili
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wana muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo ambao wamedhamiria kuondoka na alama zote tatu
Mcongomani Yannick Bangala ambaye alikosa mchezo uliopita akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano, ni miongoni mwa wachezaji wlaioingia kambini
Alipewa ruhusa kurejea kwao DR Congo kushughulikia masuala binafsi na aliingia kambini tangu juzi sambamba na Khalid Aucho, Fiston Mayele na Jesus Moloko
ADVERTISE HERE