Kikosi cha Yanga kinaanza maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa Disemba 11 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga ilirejea kutoka Mbeya jana baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza
Habari njema kwa Yanga ni kuwa majembe yake yote yapo kwa ajili ya mchezo huo wa dabi ya kwanza kwenye ligi msimu huu
Yannick Bangala amemaliza adhabu ya kadi tatu za njano, fundi Khalid Aucho na Jesus Moloko wakipumzishwa katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya Kwanza kuepusha kuonyeshwa kadi ya tatu ya njano
Wananchi wanasema hiyo Disemba 11 na ifike tu, ingawa zipo tetesi kuwa kuna watu wanataka kutumia kisingizio cha changamoto ya usafiri na wakachelewa kurudi kutoka Zambia ili mchezo huo usogezwe mbele!
ADVERTISE HERE