Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya Kwanza ambao utapigwa Jumanne katika uwanja Sokoine, Mbeya
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari leo, Nabi amesema baadhi ya wachezaji watakosekana kutokana na sababu mbalimbali
Yanick Bangala anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Yacouba Songne ni majeruhi, huku winga Jesus Moloko akipata majeraha mazoezini
Nabi amedokeza pia anaweza kukosekana kiungo Khalid Aucho ambaye bado hajapona vizuri majeraha aliyopata akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Uganda
"Hatuna hakika kama tunaweza kumtumia Aucho kutokana na kutopona vizuri majeraha. Lakini Yanick Bangala ana kadi za njano na Yacouba Sogne ni majeruhi
"Jesus Moloko ameumia sehemu ya ubavu katika mazoezi. Yanga ni kubwa kwahiyo kukosekana kwa mchezaji mmoja kunawapa wengine nafasi kuonesha uwezo wao, kimsingi tumejipanga kushinda mechi hiyo na tunajua ushindani utakuwepo," alisema Nabi