Katibu wa Baraza la Wazee la klabu ya Yanga Ibrahim Akilimali amesema yeye hapingi mabadiliko ndani ya klabu ya Yanga bali anachopinga ni klabu kukabidhiwa kwa mtu mmoja.
Katika mahojiano yake na gazeti moja la michezo nchini, Mzee Akilimali amesema anaunga mkono mabadiliko yoyote yatakayofanywa kwa mujibu wa Katiba ya Yanga na sheria za nchi.
“Nimekuwa na bahati mbaya kwa baadhi ya wanachama na viongozi, ni kutokana na kukataa katu suala la Yanga kumilikishwa mtu mmoja hilo haliwezekani na nitapinga hadi naingia kaburini, amesema Mzee Akilimali.
“Nipo tayari uanzishwe mfumo wa kampuni kama inavyotajwa katika katiba ya Yanga ibara ya 56 ambayo inasema Yanga itaanzisha kampuni ya umma ambapo wanachama wanamiliki hisa asilimia 51 na wanahisa asilimia 49.
“Lakini kwa kuwa nilikataa ndiyo naambiwa napinga mabadiliko, Yanga haikodishwi kama masufuria na kwa bahati nzuri serikali ikatusikiliza sisi watu wachache tuliopinga ukodishwaji"
Yanga tayari imeanza mchakato wa mabadiliko.
Uongozi umeunda Kamati Maalumu ya wataalamu itakayokusanya maoni ya WanaYanga kote nchi nzima kisha kushauri mfumo wa uendeshaji uliokubaliwa na WanaYanga wengi.
Kamati hiyo pia itathamini mali zote za klabu kisha kubainisha thamani halisi ya Yanga kabla ya kuingia kwenye mfumo mpya.

ADVERTISE HERE