Kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya Kwanza ambao utapigwa Jumanne, Novemba 30 kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanatarajia kuelekea mkoani Mbeya keshokutwa Jumapili tayari kwa mchezo huo ambao wamepania kurudi na alama zote tatu
Yanga iliingia kambini jana kujiandaa na mchezo huo ikiwa na kikosi chake kamili kilichomjumuisha kiungo Khalid Aucho ambaye amerejea kutoka Uganda baada ya kupona majeraha
Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amethibitisha kuwa Aucho yuko fiti na anatarajiwa kujumuishwa katika kikosi kitakachosafiri kwenda Mbeya
ADVERTISE HERE