Nabi anahitaji majembe mawili tu dirisha dogo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Nov 2021
Nabi anahitaji majembe mawili tu dirisha dogo

Imeelezwa Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amehitaji kuongezewa wachezaji wawili tu katika kikosi chake kwenye usajili wa dirisha dogo

Dirisha dogo la usajili litafunguliwa Disemba 15 2021 na kufungwa January 16 2022

Yanga ina nafasi mbili kwa ajili ya nyota wa kigeni ambapo usajili unaweza kuwa wa kujaza nafasi hizo

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, imebainisha kuwa Nabi amehitaji kuimarisha safu ya kiungo akihitaji kuletewa kiungo mchezeshaji na mshambuliaji ambaye pia anaweza kutokea pembeni

Baada ya Yacouba Songne kupata majeraha, anatarajiwa kuwa nje kwa angalau miezi mitano

Ifikapo mwezi Disemba, itabaki takribani miezi sita msimu huu kumalizika, upo uwezekano mkubwa Yacouba asitumike tena katika kipindi kilichobaki

Nafasi ya Yacouba inaelezwa kumtesa zaidi Nabi kwani ni mchezaji aliyekuwa ameingia kwenye mfumo wake na alitekeleza majukumu yake kwa ufasaha

Nabi anahitaji kupata mshambuliaji ambaye atakuwa na ubora kama aliokuwa nao Yacouba au zaidi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’