Mwamnyeto anaonyesha thamani yake uwanjani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Nov 2021
Mwamnyeto anaonyesha thamani yake uwanjani

Mwanzoni mwa msimu wapo walioamini kuwa usajili wa Yannick Bangala ungemuondoka nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto katika kikosi cha kwanza

Pamoja na ubora wake katika ulinzi, wengi hawakuwa na imani na uwezo wake katika kuanzisha mashambulizi kutokea nyuma

Lakini kwa hakika Mwamnyeto amewanyamazisha wote waliokuwa na mashaka nae

Ukizungumzia wachezaji vinara wa kupiga pasi kwenye kikosi cha Yanga, Mwamnyeto ni miongoni mwao

Na ukizungumzia wachezaji wanaopiga pasi zinazofika kwa usahihi zaidi, Mwamnyeto anaweza kuwa namba moja

Ndio! kuna mechi za ligi kuu dhidi ya Azam Fc na Ruvu Shooting, zote Mwamnyeto alikuwa na usahihi wa kupiga pasi kwa asilimia 100%

Katika michezo hiyo pia alihusika katika mabao mawili ambayo mipira ilianzia mguuni kwake

Mwamnyeto aliendeleza ubora wake hata kwenye timu ya Taifa na haikushangaza Madagascar kumfanyia 'figisu' na akakosekana kwenye mchezo waliocheza dhidi ya Tanzania kwao

Huyu ndiye mlinzi ghali zaidi mzawa, thamani yake anaionyesha uwanjani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’