Michuano ya Cosafa imenijenga - Raphael Daudi

Admin By Admin
β€’
11 Jul 2017
Michuano ya Cosafa imenijenga - Raphael Daudi
Kiungo wa Mbeya City ambaye anategemea kutua Yanga, Raphael Daudi amesema mashindano ya Cosafa yamemsaidia kumjenga kujiamini zaidi.

Katika mahojiano ya mtandao wa michezo wa MWANASPOTI, Daudi amesema uzoefu alioupata katika mashindano hayo utamjenga kuwa mchezaji bora zaidi kwenye ligi msimu ujao.

Kuhusu taarifa ya kuwa amesajiliwa na Yanga, Daudi amekiri mpango huo upo kweli lakini akagoma kuzungumza zaidi akidai bado mambo hayajakamilika.

"Mpango huo upo, ila bado sijakamilisha, nikiwa tayari nitawajulisha," amesema.

"Nimejifunza mengi katika Cosafa, kuanzia kwa wachezaji niliokuwa nao pamoja na timu zilizoshiriki jinsi ambavyo zilikuwa zinapambana kuonyesha vitu vya tofauti na kwamba soka lina heshima yake," alisema kiungo huyo.

Kitendo cha kocha wa Stars, Salum Mayanja kumpa nafasi ya kucheza ndani ya kikosi chake, alikiona kama kimefika wakati mwafaka kwake akitoa sababu ya msimu unaokuja anauona una jipya pia ushindani kuwa mkali.

"Siwezi kufunguka zaidi, msimu ujao itajulikana kwa nini nasema nimepata ujasiri na kujiamini kupitia Cosafa, iliyoniongezea hatua nyingine."
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’