Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amethibitisha kuwa kiungo fundi Khalid Aucho hatakuwa sehemu ya kikosi chake kitakachoikabili Namungo Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Ilulu, Lindi
Nabi amesema Aucho alipata majeraha kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia kati ya Mali dhidi ya Uganda na anatarajiwa kuwa nje kwa takribani siku nne
"Tulipokea taarifa kutoka kwa Daktari wa timu ya Taifa ya Uganda akitujuza kuwa Aucho alipata majeraha madogo kwenye mchezo dhidi ya Mali hivyo anahitaji walau siku nne au tano za kupumzika kabla ya kurejea uwanjani kikamilifu"
"Wachezaji wengine wapo tayari akiwemo Shabani Djuma ambaye tayari amewasili Lindi na tutakuwa nae katika mchezo siku ya Jumamosi," alisema Nabi
Nabi pia amewashukuru wadhamini wa klabu ya Yanga GSM kwa kushughulikia kikamilifu matibabu ya Yacouba Songne ambaye alirejea nchini jana baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti Tunisia
"Nwashukuru GSM, wametumia gharama kubwa kumpatia matibabu Yacouba, tunaamini atapona vizuri na kurejea uwanjani. Yacouba ni mchezaji muhimu sana kwenye timu yetu, ni mpambanaji na tungependa kuwa nae karibuni"