Tukimtaka Chama tutampata - Senzo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2021
Tukimtaka Chama tutampata - Senzo

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amesema wakimuhitaji kiungo wa RS Berkane Clatous Chama, hawatashindwa kumsajili

Chama alisajiliwa na RS Berkane akitokea klabu ya Simba katika dirisha la usajili lililopita

Senzo amesema kwa sasa hawashindwi kumpata mchezaji wanayemuhitaji, unyonge waliokuwa nao miaka ya nyuma umemalizwa na GSM

"Chama ni mchezaji bora hakuna klabu ambayo itakataa kuwa naye na kwasasa tunaiheshimu Berkane kwa kuwa bado wanamkataba naye lakini nikweli tumeulizia uwezekano wa kumpata na kama kutakuwa na uwezekano wa kumleta hapa tutamleta," Senzo aliliambia gazeti la Mwanaspoti

"Tulikuwa na unyonge huko nyuma lakini Yanga ya sasa sio rahisi ushindane nayo kutaka kumchukua mchezaji kisha ukafanikiwa kuwazidi tuna ushawishi mzuri na nguvu ya fedha"

"Unapokuwa na uongozi unaosimamia misingi mizuri ya soka na malengo kisha kubwa zaidi ukawa na watu kama GSM unakuwa na nguvu ya kutosha kumchukua mchezaji yoyote ambaye unamtaka hapa ndani na hata nje"

"Ukifuatilia wako wachezaji wengi ambao walitakiwa na klabu zingine lakini baadae wakawakosa wakizidiwa na Yanga,hii ina maana kwamba GSM ambao ni wananchi sio rahisi kuwashinda linapokuja suala la Yanga inahitaji kitu"

"Tuna benchi la ufundi lakini pia tuna kamati ya ufundi hizi idara mbili zinazoshirikiana kwa karibu kufanya kazi hii ya kutengeneza timu na utakumbuka walitulia msimu huu na sasa tunafanikiwa wachezaji tuliowasajili walitokana na mapendekezo ya makocha na watu wa ufundi," alitamba Senzo

Mjadala wa Chama kurejea Tanzania dirisha dogo uliibuliwa hivi karibuni baada ya kauli ya Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said kudokeza kuwa wakipata nafasi ya kumsajili mchezaji huyo hawatafanya makosa

Kumekuwa na taarifa kuwa RS Berkane wanamtaka kiungo Mukoko Tonombe hivyo Yanga wanaweza kumtumia kumnasa Chama

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’