Nabi kuwabadilishia mbinu Namungo Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2021
Nabi kuwabadilishia mbinu Namungo Fc

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi Jumamosi anatarajiwa kufanya mabadiliko ya lazima katika kikosi chake baada ya mshambuliaji Yacouba Songne kuumia

Yacouba yuko Tunisia akiendelea na matibabu baada ya kuumia goti katika mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting

Tayari amefanyiwa upasuaji na anaweza kuwa nje ya dimba kwa miezi mitatu au zaidi

Nabi amekiri kuwa hakupenda kumkosa mshambuliaji huyo kwenye kikosi chake kwani amekuwa na mchango mkubwa lakini anao wachezaji wengi ambao anaweza kuwatumia

"Kumkosa Yacouba ni pengo tunamuombea apone haraka, lakini maisha lazima yaendelee tunatakiwa kuwa na akili mpya ya jinsi tutakavyocheza sasa na nani ataingia eneo hilo au kwingine," alisema Nabi

Nabi mwenye uraia pacha wa Ubelgiji na Tunisia, amedokeza kuwa anawaangalia nyota wwatatu ambao ni Feisal Salum, Farid Mussa na Mukoko Tonombe kwa jinsi gani wanaweza kufanya mabadiliko chanya ya kimbinu

"Tunaweza kuangalia matumizi mengine ya Feisal kama tutaona atafaa, lakini tuna Farid nimekaa naye Zanzibar tumefanya vikao kuna mambo nataka abadilike awe na kiwango bora zaidi, wakati mwingine tuna Mukoko ni mchezaji muhimu naye tutamuangalia"

"Siwezi kuweka wazi jinsi gani tutabadilisha mbinu zetu, hayo tutayafanyia kazi huku ndani, lakini wako wengi ambao tunaweza kuangalia jinsi tutakavyowatumia ili tuwe bora zaidi"

Farid na Mukoko walikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichoshiriki maadhimisho ya mwaka mmoja wa Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi, walifanya vizuri katika michezo miwili dhidi ya Mlandege na KMKM

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’