Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea mkoani Mtwara na baadae Lindi kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumamosi, Novemba 20 katika uwanja wa Ilulu
Vinara hao wa ligi kuu ya NBC, juzi waiingia kambini Avic Town kukamilisha maandalizi ya mwisho kabla ya safari ya Lindi
Wananchi wamepata maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo ambapo wiki iliyopita walikuwa visiwani Zanzibar ambako walialikwa kwenye maadhimisho ya Mwaka mmoja Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk Hussein Ali Mwinyi
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alieleza kufurahishwa na kambi ya siku tano waliyoweka Zanzibar ambapo waliweza kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Mlandege na KMKM wakiibuka na ushindi wa 1-0 na 2-1
Nabi amepania kuvunja rekodi ya Yanga dhidi ya Namungo kwani michezo minne iliyopita baina ya timu hizo haikutoa mshindi
Namungo ni moja ya timu zilizofanya usajili mzuri ikiwa na baadhi ya wachezaji ambao wamewahi kutamba Yanga kama Obrey Chirwa, David Molinga, Abdulaziz Makame na Mohammed Issa 'Banka'
Hivyo ni mchezo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali