Yanga kuifuata Namungo Fc Jumatano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Nov 2021
Yanga kuifuata Namungo Fc Jumatano

Kikosi cha Yanga kitaondoka jijini Dar es salaam Jumatano, Novemba 17 kuelekea mkoani Lindi kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc

Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Novemba 20 kwenye uwanja wa Ilulu

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema timu imeingia kambini leo kujiandaa na mchezo huo wa mzunguuko wa sita

Bumbuli amesema wachezaji wote ikiwa pamoja na wale waliokuwa katika timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wameingia kambini leo huku nyota wengine Djigui Diarra, Khalid Aucho na Saido Ntibazonkiza wakitarajiwa kurejea usiku wa leo

Akizungumzia hali za majeruhi, Bumbuli amesema mpaka sasa ni Yacouba Songne pekee ambaye ni majeruhi akiendelea na matibabu nchini Tunisia

Bumbuli amesema Yacouba atarejea nchini baada ya siku 10 ambapo atakaporejea ndipo watafahamu muda ambao atatakiwa kukaa nje kuuguza jeraha

Dickson Ambundo na Yusufu Athumani wamepona majeraha na wako tayari kuanza mazoezi na wenzao wakati Mapinduzi Balama akisubiri ruhusa ya daktari ili kuweza kujumuishwa kikosini

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
57m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’