Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi yuko mbioni kumaliza mkataba wa kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria
Nchimbi hakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichokwenda visiwani Zanzibar katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa Serikali ya Mapinduzi chini ya Rais Dk Hussein Ali Mwinyi
Imeelezwa Nchimbi aliomba ruhusa kwenda kushughulikia matatizo binafsi lakini ni kama mchezaji huyo amejiondoa kikosini baada ya uongozi wa Yanga kutoonyesha nia ya kumuongeza mkataba
Mkataba wake na Yanga unamalizika Disemba 15 na hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kuhuisha mkataba huo
Nyota mwingine ambaye yuko mbioni kumaliza mkataba ni Adeyum Saleh ambaye pia atakuwa mchezaji huru ifikapo Disemba 15
Adeyum alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichokuwa Zanzibar na alicheza mechi zote mbili