Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema hawana muda wa kupoteza kwani baada ya kurejea kutoka visiwani Zanzibar, wanajipanga kwa ajili ya michezo inayofuata
Kaze aliyewahi kuwa mkufunzi wa Academy ya FC Barcelona nchini Canada kwa miaka mitatu, ni mtaalam hasa wa soka la Hispaniola maarufu 'tiki-taka' tena ile inayopigwa na FC Barcelona wenyewe
Amerejea Yanga kukamilisha benchi la ufundi hatari linaloongozwa na profesa Nasreddine Nabi, si mnaona Yanga ya sasa?, huwezi kuitofautisha na Barca ilee ya akina Xavi, Iniesta, Buesquet na Messi! Kabla ya kufungwa goli unapigiwa pasi 40
Sasa subiri Disemba 11, watajua-hawajui







ADVERTISE HERE