Yanga imekamilisha mechi za kirafiki visiwani Zanzibar kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMKM katika mchezo uliopigwa uwanja wa Amaan leo
Mabao ya Jesus Moloko na Fiston Mayele yametosha kuihakikishia Yanga ushindi huo ikitanguliwa kufungwa bao na KMKM kwenye kipindi cha kwanza
Yanga ilicheza mechi ya kwanza Jumanne na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mlandege hivyo leo imekamilisha mechi hizo kwa ushindi wa asilimia 100%
Wananchi bado hawafungiki kwani sasa wamecheza takribani mechi 10 zote wakishinda
Yanga inarejea Dar kukamilisha maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumamosi ya Novemba 20 uwanja wa Ilulu





ADVERTISE HERE