Kiungo wa zamani wa Yanga, Haruna Niyonzima ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Rwanda, ameingia kwenye rekodi za FIFA baada ya kuinga kwenye 'FIFA’s Century Club' amabayo inawahusisha wachezaji waliocheza michezo 100 ya timu za taifa.
Niyonzima alianza kuichezea timu yake ya taifa ya wakubwa mwaka 2006 na amefanikiwa kucheza michezo 104 na kufunga magoli 6 na kuwa mchezaji pekee aliyecheza michezo mingi kwenye timu ya taifa ya Rwanda.
Wachezaji ambao wanaingia kwenye FIFA’s Century Club ni wachezaji waliocheza michezo ya kombe la dunia, hatua ya mtoano, michezo ya kufuzu, kombe la mabara na fainali za Olimpiki kuanzia mwaka 1948 kwa waliocheza timu za wakubwa tu
Mpaka tarehe 16 oktoba 2021 ni wachezaji 575 ambao wamefikisha michezo 100 ya huku kimataifa wakiwa na timu zao kulingana na nakala iliyotolewa na FIFA ya, Rec. Sport Soccer Statistics Foundation (RSSSF).
Hongera Niyonzima kwa mafanikio hayo...!