Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi timu ya Taifa Gharib Said Mohammed 'GSM' amewaasa Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa leo kuiunga mkono Stars katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la Dunia dhidi ya DR Congo
GSM amesema ushindi katika mchezo wa leo na utakaofuata dhidi ya Madagascar unaweza kuipa nafasi Tanzania kuongoza kundi J na hivyo kuwa miongoni mwa timu 10 zitakazofuzu hatua ya mtoano ambapo timu tano zitakazoshinda mtoano zitakwenda Qatar

ADVERTISE HERE