Waacheni wawekezaji wazisaidie timu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Nov 2021
Waacheni wawekezaji wazisaidie timu

Kwa misimu minne mfululizo Yanga haikuweza kufanya vizuri kutokana na changamoto za kiuchumi

Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Wanachama na Mashabiki wa Yanga ambao wanaongoza kwa wingi

Jitihada zimefanyika, ubora wa kikosi ambacho Yanga wanacho msimu huu ni matunda ya jitihada hizo zilizopelekea GSM kuingia kuidhamini klabu pamoja na kusimamia mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji

Ni uwekezaji huohuo ambao Mohammed Dewji alifanya kwa klabu ya Simba na kufanikiwa kutawala soka la Tanzania kwa misimu minne mfululizo baada ya timu hiyo kutoka kwenye kipindi kirefu cha 'msoto'

Mafanikio katika soka yanahitaji uwekezaji, bila fedha hakuna mafanikio timu inaweza kupata, labda itokee bahati

Ni bahati mbaya sana wakati huu baadhi ya wanaojiita wachambuzi bila ya aibu wanajitokeza hadharani kupinga udhamini unaotolewa kwa baadhi ya klabu kwa sababu wanazozijua wao

Jambo hili halikutokea misimu minne iliyopita lakini wanalileta msimu huu baada ya kuona utawala wa timu wanazozishabikia umetikiswa

GSM ni mfanyabiashara na anayo haki ya kutangaza biashara yake kupitia platform yoyote ilimradi havunji sheria

Mo kupitia moja ya kampuni zake alikuwa akiidhamini Namungo Fc, GSM wameingia baada ya mkataba huo kumalizika

Udhamini unaongeza ubora wa timu na hata ligi, kwani timu zinaweza kukidhi mahitaji yao na hivyo kuwa katika ushindani mzuri

Azam wameonyesha njia, uwekezaji wao mkubwa umeleta utofauti kwenye ushindani wa ligi msimu huu

Kama kuna waliokuwa wakinufaika na udhaifu wa baadhi ya timu sasa wajipange kwa ushindani wa kweli

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’