Mjumbe wa Kamati ya Mashindano klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amesema wanazo taarifa kuwa viongozi wa klabu ya Simba mara kadhaa wameonekana nyumbani kwa wazazi wa mlinzi mahiri wa pembeni Kibwana Shomari
Hersi amesema wamezipata taarifa hizo kutoka kwa Kibwana mwenyewe na watu wa karibu ambapo amewataka Simba kufuata taratibu kama wanamtaka mchezaji huyo
"Ninazo taarifa hizo kuhusu ziara zenye nia ya kumshawishi beki wetu kijana ili ajiunge nao"
"Lakini nikwambie tu sisi kama Yanga tupo kisasa mno siku hizi hizo mbinu zao ni za kizamani mno kama wanaume kweli waje mezani walete mzigo huo ujanja ujanja wao hautawasaidia kamwe"
"Siyo Kibwana tu, tunazo taarifa kuhusu wachezaji wetu wengine kwenye safu ya ulinzi, kiungo na hata mawinga wetu"
"Sasa sijui Wana hela kiasi gani?, na Mimi siwashangai hawana scouting nzuri ya kutafuta wachezaji. Timu waliyonayo inaitwa asante Azam, sababu wachezaji wote waliotamba nao miaka mitatu iliyopita walipewa kama sadaka na Azam"
"Sasa wanawaona wamechoka wanataka tena kitonga ndiyo choko choko unaziona hizo ila kwetu hawawezi, wao waingie sokoni watafute wachezaji waunde kikosi chao hayo mengine waachane nayo Wala hawawezi kutusumbua vichwa tulishatoka huko," alisema Injinia Hersi