Kikosi cha Yanga kimerejea kambini jana kuanza maandalizi ya michezo ya ligi kuu dhidi ya Namungo Fc na Mbeya Kwanza ambazo zitapigwa baada ya mapumziko ya michuano ya Kimataifa
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za Taifa wamerejea kambini wakiongezewa nguvu na wachezaji kutoka kikosi cha timu ya vijana
Bumbuli amesema wakazi wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Mbeya ni zamu yao kuhakikisha timu inapata mapokezi mazuri na muhimu zaidi ni kuhakikisha ushindi unapatikana kwenye michezo yote miwili
ADVERTISE HERE