Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amewashukia baadhi ya wachambuzi wa soka nchini ambao kazi yao kubwa ni kuisema Yanga pamoja na GSM
Manara ametoa kauli hiyo baada ya kuibuka kwa hoja iliyotolewa na mchambuziΒ wa redio moja maarufu kuhoji kwa nini GSM wanadhamini klabu za Namungo na Coastal Union na wakat huohuo wakiwa wanaidhamini Yanga?
Ipo dhana ambayo ilianza kujengwa na viongozi wa Simba kuwa timu yao inakamiwa na wapinzani wao wakiihusisha Yanga na hoja ya mchambuzi huyo inaonekana kuwa kwenye mlengo huo huo hasa baada ya Simba kushindwa kuifunga Coastal Union na kupata ushindi dhidi ya Namungo kwenye dakika ya 96, dakika 2 nje ya muda wa nyongeza (dakika 4)
Simba pia walishindwa kupata ushindi dhidi ya Biashara United,wakapata ushindi wa tabu kwenye michezo dhidi ya Dodoma Jiji na Polisi Tanzania
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Manara ameandika haya;