Yameshazungumzwa mengi kuhusu Yannick Bangala Litombo, itoshe kusema usajili wa Mcongomani huu umekuwa na thamani kubwa kwa Yanga
Huwezi kutenganisha ubora wa Yanga na umahiri wa Bangala katika eneo la kiungo
Anafanya kazi mbili muhimu kwa umakini sana, kuchezesha timu na kuvuruga mipango ya wapinzani
Katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao Yanga ilipata ushindi wa mabao 3-1 Bangala alipiga pasi 108
Idadi ya pasi zake ni karibu nusu ya pasi zote ziilizopigwa na Ruvu Shooting!
Katika mchezo dhidi ya Azam Fc Bangala alipiga pasi 66 akiwa nyuma ya Khalid Aucho ambaye alipiga pasi 82
Aucho hakucheza mechi dhidi ya Ruvu Shooting baada ya kupata majeraha mazoezi
Nafasi yake ilichukuliwa na Mukoko Tonombe ambaye aliifungia Yanga bao la tatu
Bangala na Aucho wananogesha 'tiki-taka' linalopigwa na Yanga msimu huu