Timu ya ushindi haibadilishwi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Nov 2021
Timu ya ushindi haibadilishwi

Kwa sasa benchi la ufundi la Yanga chini ya Kocha Nasreddine Nabi wanafanya vizuri sana katika uchaguzi wa wachezaji wa kikosi cha kwanza

Yawezekana wapo baadhi ya wachezaji vipenzi wa mashabiki hawapati nafasi kulingana na vile benchi la ufundi linapanga, halipaswi kuwa jambo lenye mjadala kwa sababu timu inafanya vizuri

Utamaduni wa makocha wote duniani, hawabadili timu zinazowapa matokeo labda itokee changamoto ya kadi na majeruhi

Nabi tayari amepata kikosi chake cha kwanza ambacho kimempa ushindi katika michezo minne mfululizo kwenye ligi

Hana sababu ya kufanya mabadiliko ambayo yanaweza kuathiri uchezaji wa timu yake

Wachezaji wanaoanza sasa kwenye kikosi cha kwanza wamezoeana, kila mmoja anafahamu wapi anapaswa kuwa na wakati gani

Kuna wachezaji kama Saido Ntibazonkiza, Mukoko Tonombe, Heritier Makambo, Zawadi Mauya na wengine wanalazimika kusubiri nje 

Sio kwa sababu hawana uwezo, lahasha, kwa sababu kuna wenzao wanafanya vizuri katika nafasi wanazocheza

Pia kuna changamoto ya wachezaji nane wa kigeni ambao wanapaswa kuanza katika mchezo mmoja

Nyota wa kigeni wengine wanalazimika kubaki nje kutokana na kanuni hii

Makambo na Saido hawakuwa sehemu ya kikosi kilichoikabili Azam Fc Jumamosi, pengine leo wanaweza kubaki nje katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting pia

Makambo amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi mbele ya Fiston Mayele ambaye amefunga katika mechi mbili zilizopita

Saido hajaweza kuingia katika kikosi cha mechi kabisa kutokana na nafasi anayocheza kuwa na wachezaji wanaofanya vizuri

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’