Vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga leo wako uwanjani Benjamin Mkapa kuumana na Ruvu Shooting katika mwendelezo wa ligi hiyo
Wananchi ndio timu pekee ambayo mpaka sasa imepata ushindi wa asilimia 100% katika michezo minne waliyocheza
Wanasaka ushindi wa tano kufikisha alama 15 ambazo zitaendelea kuwachimbia kileleni mwa msimamo wa ligi
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 12:15 jioni, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi
Bumbuli amesema mwendo ni uleule, mashabiki watapata burudani pamoja na kushangilia ushindi
ADVERTISE HERE