Obrey Chirwa amebeba lawama ya 'kuirudisha' Yanga nyumbani baada ya kukosa mkwaju muhimu wa penati dhidi ya URA kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi.
Hata hivyo kwa upande mwingine kutozingatiwa kwa sheria za penati na mwamuzi wa mchezo huo ni jambo linalopaswa kumulikwa.
Kabla Chirwa hajapiga penati mlinda lango wa URA anaonekana kusogea mbele kwa hatua mbili kinyume na sheria inavyoelekeza.
Cha kushangaza Mwamuzi alimuona kipa akitoka kwa kuwa alikuwa karibu nae kabisa. Ilitegemewa angeamuru penati hiyo irudiwe.
Sheria za FIFA kwenye upigaji wa penati zimebainisha kuwa mlinda lango haruhusiwi kusogea mbele ya goli wakati mpira wa penati ukipigwa.
Mlinda Lango anaruhusiwa kusogea kulia/kushoto kwake akifuata mstari unaounganisha milingoti miwili ya goli na si kusogea mbele.
Sheria inatamka bayana kama mlinda lango atasogea mbele, kama mpigaji atakosa mwamuzi ataamuru penati hiyo irudiwae lakini kama atafunga basi bao litakubaliwa.
Waamuzi wakongwe wamemkosoa mwamuzi wa mchezo huo kwa kutoamuru penati ya Chirwa irudiwe.
Miongoni mwa waliotoa maoni yao ni Katibu wa Kamati ya waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye pia ni mwamuzi mstaafu, Kenedy Mapunda.
Mapunda anasema kisheria penalti ya Chirwa ilipaswa kurudiwa kutokana na golikipa huyo kutoka kwenye mstari wa goli kwa hatua mbili mbele kabla ya kupigwa kwa mpira.
"Kosa la kwanza ni kitendo cha golikipa kutoka mbele kabla ya mpira kupigwa, lakini pia mwamuzi alipaswa kuamuru penalti ile kurudiwa kwa mujibu wa kanuni," alisema Mapunda.
Kauli ya Mapunda pia iliungwa mkono na mwamuzi mstaafu, Omari Abdulkadir, ambaye alisema waamuzi wa mechi ya URA dhidi ya Yanga hawakutenda haki kwenye penalti ya Chirwa.
"Golikipa anaruhusiwa kusogea akiwa kwenye mstari wake kwenda kushoto au kulia lakini haruhusiwi kusogea kwenda mbele," Abdulkadir alisema na kuongeza kuwa:
Γ’β¬ΕSheria inaweka wazi. Kitendo kama kile mwamuzi alitakiwa kutoa uamuzi wa penalti irudiwe kama mpigaji alikosa, lakini kama lingeingia goli, goli lingekubalika.
"Niliuangalia mpira na kitendo kile nilikiona, nilifikiri penalti ingerudiwa... unajua golikipa siyo asikie filimbi ndiyo atoke kwenye mstari wake, hapana hata kama filimbi imepigwa anatakiwa asitoke kwenye mstari wa goli mpaka mpira upigwe."

ADVERTISE HERE