Bila shaka maafande wa Ruvu Shooting ujumbe umewafikia kuwa ni zamu yao 'kupapaswa' na Wananchi pale dimba la Benjamin Mkapa!
Ndio wanafuatia kwenye ratiba ambapo keshokutwa Jumanne watakuwa wageni wa Yanga pale uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga hii ni sawa na gari lililokata breki kwenye mteremko, yaani yeyote anayekuja mbele yake haponi!
Ushindi wa mabao 2-0 waliopata Yanga dhidi ya Azam Fc jana ni ushindi wa tano mfululizo, wakishinda mechi nne za ligi na mchezo mmoja wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba
Sasa Wananchi wamecheza dakika 540 pasipo kuruhusu bao kutikisa nyavu zao huku wenyewe wakifunga mabao saba
Wananchi wako kileleni mwa msimamo wa ligi wakijikusanyia alama 12
Zamu yetu mzee? pic.twitter.com/M9zbxJUHdn
— Ruvu Shooting Football Club (@Ruvu_shootingFc) October 30, 2021
ADVERTISE HERE