Nyie..nyie..hawaogopi?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Oct 2021
Nyie..nyie..hawaogopi?

Azam Fc walisifiwa sana baada ya kuonyesha kiwango bora dhidi ya Pyramids kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho kule Misri licha ya kufungwa bao 1-0 na kuondoshwa katika michuano hiyo

Pengine ndio sababu wachambuzi wengi waliamini Azam Fc ingeweza kuisumbua Yanga bila ya kujali ubora walionao Yanga wakati huu

Sikia hii, mbele ya Azam Fc, Yanga imepiga zaidi ya 500 katika mchezo huo ambao Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 2-0

Yanga ilikuwa bora katika kutengeneza mashambulizi na ilikuwa bora katika ulinzi pia

Haikuwa rahisi kwa Azam Fc kupata mwanya wa kuipenya ngome ya Yanga ndio maana walitengeneza nafasi chache sana

Hii Yanga imeiva hasa, shukrani kwa usajili makini uliofanywa na GSM, umeanza kulipa

Hawa watu wawili Yannick Bangala na Khalid Aucho, wajengewe masanamu mapemaa

Aucho anaufanya mchezo wa mpira wa miguu uonekane rahisi sana wakati Bangala ni kama mlinzi wa zamu, hakuna ruhusa ya kupita getini kuingia ndani

Mayele atafunga kila mechi, msimu huu anafunga zaidi ya mabao 25, tuendelee kumuhesabia tu

Jesus Moloko anaendelea kuonyesha utofauti wake na Tuisila Kisinda, ana shabaha, anaweka kambani akipata nafasi

Yacouba wengi hawamuelewi lakini ni jembe hasa, mikimbio yake inawasumbua sana walinzi wa timu pinzani

Anaweza asifunge lakini anatengeneza nafasi, hivi mnajua mabao yote yaliyofungwa na Moloko ameyapika Yacouba?

Yanga hii imekamilika kama timu, huu ni msimu wa furaha kwa Wananchi...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
39m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’