Mpya

Match Day : Yanga vs Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Oct 2021
Match Day : Yanga vs Azam Fc

Kikosi cha Yanga leo kitashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Azam Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya NBC

Wananchi wenyewe wanasema kukaa bila kuishuhudia Yanga unaweza kuugua! Zimepita siku 11 tangu walipocheza dhidi ya KMC na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 mkoani Ruvuma

Leo wataishuhudia timu yao katika mchezo dhidi ya Azam Fc, pale dimba la Mkapa kuanzia saa moja usiku

Ni mchezo ambao utakuwa na ushindani mkali kutokana na historia ya timu hizi kila zinapokutana

Mpaka sasa hakuna timu iliyoshinda mechi nyingi zaidi ya mwenzake na kwa wastani, kila msimu zimekuwa zikigawana matokeo

Msimu uliopita Yanga ilishinda mchezo wa duru ya kwanza na Azam Fc wakashinda mchezo wa duru ya pili

Hata hivyo huu ni msimu mwingine, Yanga imebadilika lakini hata Azam Fc wamebadilika pia

Wananchi wanasaka ubingwa wa 28 wa ligi kuu baada ya kuukosa kwa misimu minne mfululizo, wamedhamiria kutimiza kusudio hilo

Ili kuwa bingwa unapaswa kukusanya alama nyingi kuliko wengine wote na muhimu unapaswa kupata alama nyingi dhidi ya wapinzani wako katika mbio za ubingwa

Hivyo ni mchezo ambao Yanga inahitaji kuondoka na alama zote tatu pamoja na kuwa hautakuwa mchezo mwepesi

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wachezaji wako tayari na wanajua aina ya mchezo wanakwenda kucheza dhidi ya Azam Fc

Hii ni siku ya burudani kwa mashabiki wa Yanga kwani kabla ya mchezo watapata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali

Hivyo kwa mashabiki ni vyema wakawahi mapema uwanjani kwani kuna mambo mengi yameandaliwa kwa ajili yao

More Stories

Yanga Complete Preparations Ahead of Gaborone United CAF Champions League Clash
Yanga Complete Preparations Ahead of Gaborone United CAF Champions League Clash
4h ago
READ MORE β†’
Toure Confident His Goals Will Come as He Adapts to Life at Yanga
Toure Confident His Goals Will Come as He Adapts to Life at Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Mngqithi Named NBC Premier League Coach of the Month for August
Mngqithi Named NBC Premier League Coach of the Month for August
11h ago
READ MORE β†’
Gomez Calls on Yanga Fans to Fill Azam Complex Ahead of Gaborone United Decider
Gomez Calls on Yanga Fans to Fill Azam Complex Ahead of Gaborone United Decider
11h ago
READ MORE β†’
Mngqithi Warns Yanga Against Complacency Ahead of Gaborone United Decider
Mngqithi Warns Yanga Against Complacency Ahead of Gaborone United Decider
11h ago
READ MORE β†’
Mngqithi Reveals Aziz Ki’s Fitness Limit Ahead of Gaborone United Return Leg
Mngqithi Reveals Aziz Ki’s Fitness Limit Ahead of Gaborone United Return Leg
14h ago
READ MORE β†’
Yanga Fans Snap Up Tickets Ahead of Gaborone United Decider
Yanga Fans Snap Up Tickets Ahead of Gaborone United Decider
15h ago
READ MORE β†’
Mngqithi Believes Yanga Can Reach CAF Champions League Final
Mngqithi Believes Yanga Can Reach CAF Champions League Final
16h ago
READ MORE β†’
Today's Newspapers, Friday, September 11, 2026
Today's Newspapers, Friday, September 11, 2026
18h ago
READ MORE β†’
Pacome Visits Yanga Teammates as He Continues Recovery from Injury
Pacome Visits Yanga Teammates as He Continues Recovery from Injury
1d ago
READ MORE β†’