Tuko tayari kuikabili Azam Fc - Hafidh

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Oct 2021
Tuko tayari kuikabili Azam Fc - Hafidh

Kuelekea mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa, kikosi cha Yanga leo kinakamilisha maandalizi yake ya mwisho tayari kwa mchezo huo wa 'kukata na shoka'

Wananchi wamejichimbia kambini Avic Town kwa takribani siku 10 baada ya mchezo dhidi ya KMC uliopigwa Songea na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema wachezaji wanaendelea vyema na wako tayari kupambana kwa ajili ya kuondoka na ushindi katika mchezo huo

Saleh alisema kila mchezaji wa Yanga anafahamu umuhimu wa mechi hiyo na wamejiandaa kuendelea kuwapa furaha wanachama na mashabiki wao

"Malengo yetu ni kutwaa ubingwa, na ili uwe bingwa ni lazima upate pointi nyingi, tunahitaji ushindi ili tuendelee kujiimarisha katika msimamo wa ligi, tunajua haitakuwa mechi rahisi kwa sababu wenzetu pia wamejipanga na wana kikosi imara," Saleh alisema

Akizungumza kwenye Mkutano na Wanahabari, Mhamasishaji wa Yanga Haji Manara alisema mchezo dhidi ya Azam Fc unaweza kuwa 'dabi' bora ya Dar es salaam huku akibainisha kuwa Azam Fc ndio timu inayoweza kuwapa changamoto katika mbio za ubingwa

"Hii ndio dabi ya Dar es salaam, kwangu mimi naona sisi Yanga na Azam Fc ndio timu zilizofanya usajili mzuri na wanaweza kutupa ushindani katika mbio za kuwania ubingwa"

"Hata hivyo Yanga ni kitu kingine, msimu huu tumedhamiria kushinda ubingwa, kwa uwezo wa Mwenye ez Mungu tutashinda"

"Nawaambia mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani kuwashangilia wachezaji wetu. Kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii kabla ya mchezo. Huu ni utaratibu ambao tunaanza kuutumia Jumamosi na tutauendeleza katika michezo yote tutakayocheza nyumbani"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’