Afisa Habari wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amesema wamefanya uwekezaji mkubwa katika timu ili kuhakikisha wanafikia malengo
Katika msimu huu, kikosi cha Yanga kimeonekana kuimarika kutokana na usajili mkubwa uliofanywa dirisha lililopita
Bumbuli amesema wamedhamiria kushinda mataji yote ya ndani na kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa
"Tumefanya usajili mzuri kwa kuchukua wachezaji wazuri, benchi la ufundi likiongozwa na Nabi lakini ameongezeka Kaze ambaye alikuwepo msimu uliopita"
"Pia tumemrudisha Zahera kwa ajili ya kuwapika vijana. Malengo ambayo tumeyakusudia ni mataji ya ndani, tumewekeza nguvu tunapokijenga kikosi imara kichukue Ligi Kuu, Azam Sports Federation na Mapinduzi Cup"
"Msimu ujao kikosi kitakuwa kimeimarika zaidi tutakiongezea nguvu kidogo kuelekea kwenye michuano ya kimataifa," alisema Bumbuli
Jumamosi Wananchi wanashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC