Mjadala kuhusu nembo ya Mdhamini wa Ligi Kuu ya NBC na klabu ya Yanga kugomea rangi yake, umekuwa mkubwa na kishabiki zaidi
Lakini Bodi ya Ligi imebainisha kuwa haina tatizo lolote na makubaliano ambayo NBC watafikia na klabu kuhusu rangi ya nembo
Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo amesema Bodi itasimamia kanuni inayoelekeza timu kuvaa jezi yenye nembo ya mdhamini lakini hawatapinga makubaliano binafsi kati ya Mdhamini na Klabu
"Sisi tunasimamia kanuni na mkataba unazitaka timu kuvaa jezi zenye nembo ya Mdhamini. Suala la rangi ni timu kuongea na Mdhamini Sisi Bodi tunasimamia kanuni na mkataba unahitaji timu ivae nembo bila kujali ni rangi gani kikubwa makubaliano yao," alisema Kasongo
Yanga ilishafanya majadiliano na NBC, kesho kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc wale 'wapiga kelele' wataiona rangi ya nembo ya NBC ambayo iko kwenye jezi za Yanga
Lakini wasitarajie kuona 'doa jekundu' kwenye jezi ya mabingwa hao wa kihistoria