Baada ya mwaka mmoja, hatimae Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kesho Jumanne itatoa hukumu ya kesi ya Yanga dhidi ya mchezaji Bernard Morrison
CAS iliahirisha kutoa hukumu ya kesi hiyo mara mbili lakini wakaahidi kuwa hukumu hiyo sasa wataitoa Oktoba 26, siku ya kesho Jumanne
Kesi hii imechukua muda mrefu hata kupelekea baadhi ya mashabiki kupoteza imani kuwa pengine haipo
Lakini jambo la uhakika ni kesi ipo na kesho ndio siku ambayo hatma yake itafahamika
Kwani baada ya kuahirisha kutoa hukumu mara mbili, CAS hawatarajiwi kuahirisha tena
ADVERTISE HERE