Yanga ilitolewa na Rivers United kwenye hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa kwa kufungwa katika michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini
Ni matokeo ambayo hayakushangaza wengi kwa sababu timu haikuwa na maandalizi ya kutosha
Michuano ya ligi ya mabingwa sio lele mama, unahitaji kuwa na timu imara kuweza kufanya vizuri
Katika msimu uliopita michuano hiyo ilikuwa ikionekana rahisi kwa sababu nchi nyingi hazikuwa na ligi kutokana na changamoto ya corona
Lakini msimu huu kila mmoja amerejea akiwa amejipanga na haishangazi kuona watani zetu wameondoshwa na timu kutoka Botswana, tena kwa kufungwa mabao mengi nyumbani
Yanga inajipanga kurejea kwenye michuano hiyo msimu ujao ikiwa imara. Wananchi watatumia msimu huu wote kujiweka sawa
Naamini kwa kikosi hiki cha Kocha Nasreddine Nabi, wakati huo kitakuwa kimeiva kwelikweli na hakika tutaweza kuzungumzia kwenda mbali zaidi ya hatua ya makundi
Mpango ulipo mbele kwa sasa ni kushinda ubingwa ili kujihakikishia tiketi ya kushiriki michuano hiyo msimu ujao