Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanasubiri kukamilka kwa mchakato wa kuweka nembo ya wadhamini wa ligi kuu (NBC) kwenye jezi
Hata hivyo Bumbuli amesema kwa utamaduni wa Yanga, hakuna nafasi ya 'doa jekundu' katika jezi zao, jambo hilo linafahamika kwa miaka mingi hivyo wanatarajia wadhamini watazingatia
"Hatukutumia nembo ya Mdhamini kwenye mchezo wetu dhidi ya KMC kwa sababu mchakato wa ku-brand jezi ulichelewa, tulipewa taarifa Ijumaa na tukaambiwa jezi tutazipata Jumatatu wakati sisi tuliondoka Jumapili kuelekea Songea, ndio maana kwenye mchezo huo tulitumia jezi yetu ya tatu"
"Muhimu kwa utamaduni wetu Yanga haturuhusu doa jekundu katika jezi zetu, hili ni jambo linalofahamika, naamini wadhamini watazingatia. Kwani nafahamu Mdhamini anapaswa kuwa na nembo zaidi ya moja, ili pale inapotokea ukinzani kusitokee changamoto"
"Tukiwa brand kubwa zaidi Tanzania, tungependa kuona Mdhamini ananufaika kushirikiana nasi, hatutarajii kutokea kwa changamoto yoyote katika hili," alisema Bumbuli