Baada ya Yanga kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, kuna watu walianzisha propaganda kuwa uongozi ulikuwa umempa Kocha Nsareddine Nabi mechi mbili
Hata hivyo taarifa hizo zilikanushwa haraka sana na uongozi wa Yanga wakasisitiza kuwa na imani na kocha huyo mwenye uraia pacha ya Tunisia na Ubelgiji
Nabi anabebwa na takwimu zake nzuri tangu alipojiunga na Yanga mwishoni mwa mwezi April mwaka huu
Amekuwa na mwenendo mzuri katika michezo 18 aliyoiongoza Yanga
Ameshinda michezo 12, ametoka sare mechi mbili na kupoteza mechi nne tu ikiwa ni pamoja na mechi za ligi ya mabingwa msimu huu dhidi ya Rivers United
Yaani kwenye ligi kuu tangu alipotua Yanga amepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Azam Fc ambao ulikuwa mchezo wake wa kwanza April 23
Amepata matokeo ya sare dhidi ya Namungo Fc na Dodoma Jiji huku akipoteza mchezo mmoja wa fainali kombe la FA dhidi ya Simba
Nabi aliongoza vipigo viwili dhidi ya Simba, ushindi wa ligi kuu msimu uliopita na Ngao ya Jamii msimu huu
Ameanza vyema msimu huu akishinda mechi zote tatu za mwanzo pasipo timu yake kuruhusu bao
Kwa hakika baada ya bandika bandua ya makocha, hapa kwa Nabi Yanga imepata kocha wa mpira...!