Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC hapo jana, kikosi cha Yanga kinarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Azam Fc
Vinara hao wa ligi kuu ya NBC watacheza mechi mbili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya ligi kusimama kupisha kalenda ya FIFA
Mchezo dhidi ya Azam Fc utapigwa Oktoba 30 na kisha kufuatiwa na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa Novemba 02
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema kikosi kimeendelea kuimarika huku wakipata matokeo mazuri
"Mechi ya tatu (ugenini), ushindi wa tatu, tunaimarika kila siku kama timu. Tungali na vitu vingi vya kuboresha. Tunarudi nyumbani kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu unaofuata dhidi ya Azam tarehe 30 Oct. Ligi ingali mwanzoni," alisema Kaze
Akijibu kauli za wanaodai wachezaji wa Yanga hawakuwa na pumzi kwenye kipindi cha pili, Kaze alisema baada ya kufunga mabao mawili hawakuwa na sababu kukimbia kimbia kama walivyoanza mchezo huo
"Sio kweli kwamba wachezaji wanakata pumzi, Hatukuwa na sababu ya kuendelea kukimbia kimbia uwanjani kwakuwa tumeshapata ushindi wa goli 2 ndani ya dakika 15"
Pamoja na baadhi ya wachambuzi kuja na wimbo huo wa 'kukata upepo' katika kipindi cha pili, Yanga imecheza mechi nne pasipo kuruhusu bao