Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya KMC ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Majimaji, Songea
Yanga iliwasili Songea mapema jana na jioni ikafanya mazoezi yake ya kwanza kujiandaa na mchezo huo
Hafidh amesema wachezaji wote 24 waliosafiri na timu wako tayari kwa mchezo huo ambao wamedhamiria kuondoka na alama zote tatu
"Tumefanya mazoezi yetu ya kwanza baada ya kufika hapa (Songea). Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri"
"Tunawaheshimu KMC kwani ni timu nzuri lakini tumejipanga kuendeleza mwanzo mzuri kwenye ligi msimu huu"
"Baadhi ya wachezaji wamebaki jijini Dar es salaam kwa sababu bado hawako sawa isipokuwa Saido Ntibazonkiza ambaye hakufanya mazoezi na wenzake tangu amerudi kutoka kuitumikia timu yake ya taifa ya Burundi," alisema Hafidh
Yanga leo inatarajiwa kukamilisha maandalizi ya mwisho kwenye uwanja wa Majimaji tayari kwa mchezo huo ambao utapigwa kuanzia saa kumi Alasiri