Nabi aandaa mkakati wa kuwamaliza KMC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Oct 2021
Nabi aandaa mkakati wa kuwamaliza KMC

Jana Yanga ilirejea mazoezini ikiwa na kikosi kamili kukamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa uwanja wa Majimaji Jumanne, Oktoba 19 2021

Baada ya kujifua kwa wiki nzima pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi aliwapa mapumziko ya siku mbili wachezaji ambao hawakuwa na majukumu ya timu za Taifa

Sasa wameungana na wenzao waliokuwa katika timu za Taifa, wakianza na mazoezi makali ya ufukweni na Gym

Nabi amesema program ya mazoezi anayowapa wachezaji wake ni sehemu ya mpango wake kuelekea mchezo dhidi ya KMC

"Tunafanya mazoezi ya aina mbalimbali, kwa sasa tumezingatia zaidi kujenga stamina, wachezaji wanatakiwa kuwa imara, ligi ni safari ndefu, wanatakiwa wawe katika kiwango cha juu cha kushindana kuanzia mwanzo hadi mwisho wa msimu"

"KMC ni moja ya timu ambazo wachezaji wake wanatumia nguvu, ninajua namna ambavyo tutawakabili, naamini tutapata kile ambacho tunakihitaji kama timu," alisema Nabi

Aliongeza kurejea kwa wachezaji wake waliokuwa kwenye timu za taifa mbalimbali kutawanufaisha kwa sababu huko pia walikuwa kwenye mazoezi magumu na yenye kuhitaji kuzalisha matokeo chanya.

"Tunahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kutuweka kwenye nafasi nzuri, tukipata matokeo mazuri yatatuweka kwenye nafasi nzuri ya kuelekea katika maandalizi ya kuwakabili Azam, mechi zote zinahitaji kuwa na kikosi imara"

Yanga inatarajiwa kuelekea Ruvuma keshokutwa Jumapili tayari kwa mchezo huo ambao utapigwa Jumanne

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’