Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema wachezaji waliokuwa na majukumu ya timu za Taifa wameungana na wenzao kukamilisha maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa Jumanne ijayo mkoani Ruvuma
Hafidh amesema wachezaji waliingia kambini jana isipokuwa mlinda lango Djigui Diarra ambaye alikuwa na changamoto ya pasipoti, yeye atawasili nchini leo
Aidha mchezaji majeruhi ni mmoja tu, Dickson Ambundo ambaye aliumia mkono kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU
ADVERTISE HERE