Azam FC itaumana na URA katika mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Singida United bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa Jumatano usiku.
Bao pekee la Azam FC lilifungwa na Iddi Chilunda kwenye dakika ya 78.
Mapema leo URA iliitoa Yanga kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya matokeo ya sare ya 0-0.
Sasa mchezo wa fainali utazikutanisha kwa mara ya pili URA na Azam FC timu zilizokuwa kundi moja la B.
Wakati zilipokutana kwenye hatua ya makundi URA iliichapa Azam FC bao 1-0 hivyo kuufanya mchezo huo wa fainali kuwa mchezo wa kisasi kwa Azam FC.
Azam FC ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo na wana nafasi ya kulibakisha taji hilo Chamazi kwa mwaka wa pili mfululizo.

ADVERTISE HERE