Oktoba 19 Yanga itashuka kwenye uwanja wa Majimaji Songea kuikabili KMC katika mchezo wa NBC Premier League
Wengi wameshtushwa na KMC kupeleka mchezo huo Ruvuma, lakini hii sio mara yao ya kwanza kuuhamisha mchezo dhidi ya Yanga kutoka uwanja wa Benjamin Mkapa
Msimu uliopita waliupeleka jijini Mwanza, uwanja wa CCM Kirumba lakini Yanga iliweza kushinda mchezo huo kwa mabao 2-1
Haishangazi, kwani ni hawahawa KMC msimu wa 2018/19 walizawadiwa Tsh Milioni 20 na aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda baada ya kuifunga Yanga
Wananchi wana dhamira ya kushinda ubingwa msimu huu, hivyo wanapaswa kuwa tayari kucheza katika mazingira yoyote
Ubingwa hautapatikana kwa kushinda uwanja wa Benjamin Mkapa pekee
Yanga itakwenda kucheza uwanja wowote na lengo la kushinda kila mchezo litabaki vilevile