Nahodha Msaidizi wa Yanga Mukoko Tonombe amerejea akiwa 'fit' baada ya kukosa mechi tatu za mwanzo wa msimu akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Simba mwishoni mwa msimu uliopita
Juzi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, Mukoko alikuwa bora eneo la kiungo akishirikiana vyema na Farid Mussa ambaye msimu huu Kocha Nasreddine Nabi anamtumia zaidi katika dimba la kati
Kurejea kwa Mukoko kunaongeza vita katika eneo la kiungo benchi la ufundi likiwa na jukumu la kuamua nani aanze kati ya Khalid Aucho, Mukoko, Zawadi Mauya na Yannick Bangala ambaye hata hivyo anaweza kutumika kama mlinzi wa kati
Itoshe kusema kwa sasa Yanga ndio timu yenye safu bora ya kiungo