Jana mshambuliaji wa Yanga Yacouba Songne alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Burkina Faso kilichoikabili Djibouti katika mchezo wa kufuzu kombe la Dunia
Katika mchezo huo ambao Burkina Faso walishinda mabao 2-0, Yacouba aliingia kwenye dakika ya 72 akichukua nafasi ya Mohammed Konate
Yacouba ni mmoja wa wachezaji tisa wa Yanga waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa
Wamekamilisha majukumu hayo sasa wanarejea 'kukiwasha' ndani ya kikosi cha Yanga
ADVERTISE HERE