Godfrey Nyarko ni kiungo mshambuliaji ambaye yuko ndani ya kikosi cha Yanga tangu mwishoni mwa mwezi August akitokea klabu ya Medeama
Nyarko aliletwa kwa dhumuni la kusajiliwa lakini Kocha Nasreddine Nabi alihitaji kujiridhisha na uwezo wake kabla ya kupewa mkataba
Hivyo pamoja na kuwa bado hajasajiliwa, ameendelea kujifua na kikosi cha Yanga tangu wakati huo kukiwa na uwekano wa kusajiliwa katika dirisha dogo mwezi Disemba
Yanga imesaji nyota 10 wa kigeni hivyo bado ina nafasi za kusajili wachezaji wengine wawili
Jana kwenye mchezo dhidi ya JKU, Nyarko alipata nafasi ya kucheza katika kipindi cha pili akionyesha uwezo mzuri
Mahiri katika matumizi ya mguu wa kushoto na hatari sana akitokea upande wa kulia
Pia ameonyesha umahiri wa kupiga pasi na mipira iliyokufa
Nafikiri kwa benchi la ufundi kuwa nae kikosini kwa zaidi ya mwezi mmoja, ni wazi wameridhishwa na uwezo wake, sasa anaendelea kuzoeana na wenzake ili pale atakaposajiliwa asiwe mgeni
Nyarko ni mchezaji mzuri ambaye ataisaidia Yanga katika kampeni yake ya kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu