Yanga imethibitisha kuwa mlinzi wake wa kushoto Yassin Mustafa amepona majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani miezi sita
Yassin ameanza mazoezi na wachezaji wengine pamoja na kuwa bado anapewa program maalum ili kumuimarisha zaidi
Kurejea kwake kunaongeza ushindani kwenye safu ya ulinzi upande wa kushoto
Kabla ya kupata majeraha Yassin ndiye alikuwa chaguo la kwanza msimu uliopita
Alipoumia Adeyum Saleh alicheza mechi zote zilizosalia kukamilisha msimu
Yanga ikalazimika kusajili mlinzi mwingine wa kushoto David Bryson baada ya Yassin kuchelewa kupona majeraha
Bahati mbaya Bryson naye alisajiliwa huku akiwa majeruhi na hivyo kumfanya kukosa mechi za mwanzoni kwenye ligi ya mabingwa
Kocha Nasreddine Nabi akalazimika kumrudisha Kibwana Shomari upande wa kushoto baada ya usajili wa Djuma Shabani
Katika mechi chache alizocheza katika upande wa kushoto, Kibwana amekuwa na kiwango bora sana
Sasa Yassin amrejea, Bryson na Adeyum nao wapo, je wataweza kumuhamisha Kibwana namba?
Mwisho wa siku yule atakayefanya vizuri katika kiwanja cha mazoezi ndiye atakayekuwa na nafasi ya kucheza